Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Rais Bush amaliza ziara yake barani Ulaya
  •  2007/06/12
    Tarehe 4 hadi 11 Juni, rais Bush wa Marekani kwa nyakati tofauti alitembelea nchi 6 za Ulaya ambazo ni Czech, Ujerumani, Poland, Italia, Albania na Bulgaria. Wakati wa ziara yake hiyo alihudhuria mkutano wa wakuu wa kundi la nchi nane uliofanyika nchini Ujerumani, na aliafikiana na nchi za Ulaya katika suala la kuwa joto kwa hali ya hewa duniani. Wakati huohuo rais Bush alizishawishi nchi za Ulaya ya mashariki kuunga mkono mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa Marekani, na kuendelea kuweka shinikizo kwa Russia.
  • Mazungumzo kati ya Iran na Umoja wa Ulaya yatakwamua utatuzi wa suala la nyuklia la Iran?
  •  2007/06/11
    Naibu katibu wa kamati ya usalama ya taifa ya Iran Bw. Javad Vaidi pamoja na msaidizi wa Bw. Javier Solana, mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama, wamekuwa na mazungumzo tarehe 11 mwezi Juni.
  • Rais Hu Jintao ahudhuria Mkutano wa mazungumzo kati ya kundi la nchi nane na viongozi wa nchi zinazonedelea
  •  2007/06/09
    Mkutano wa mazungumzo kati ya kundi la nchi nane na viongozi wa nchi zinazoendelea ulifanyika tarehe 8 Juni huko Heiligendamm, kaskazini mwa Ujerumani. Mkutano huo ulijadili hasa masuala kuhusu uchumi wa dunia na mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Mkutano wa kundi la nchi 8 umefikia maoni ya pamoja isivyotarajiwa
  •  2007/06/08
    Viongozi wa kundi la nchi 8 tarehe 7 Juni walifanya Mkutano huko Heligendamm, Ujerumani, wakijadili masuala mengi yakiwemo uhifadhi wa hali ya hewa, usalama wa nishati, misaada kwa Afrika, na maendeleo ya uchumi wa kimataifa. Katika hali isiyotarajiwa na watu , kundi hilo la nchi 8 lilifikia maoni ya pamoja kuhusu masuala mengi makubwa ambayo yalidhaniwa kuwa na maoni tofauti.
  • Rais wa China na viongozi wa India, Brazil, Afrika ya kusini na Mexico wakutana
  •  2007/06/08
    Rais Hu Jintao wa China tarehe 7 Juni huko Berlin, mji mkuu wa Ujerumani alikutana na waziri mkuu wa India Manmohan Singh, rais Luiz Lula da Silva wa Brazil, rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini na rais Felipe Calderon wa Mexico walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa mazungumzo kati ya kundi la nchi 8 na viongozi wa nchi zinazoendelea, ambapo walibadilishana maoni kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na mazungumzo ya Doha, na masuala mengine, baadaye Mkutano huo ulitoa taarifa ya pamoja.
  • Masuala manne muhimu ya mkutano wa kilele wa nchi nane mwaka huu
  •  2007/06/07
    Wakuu wa nchi wa kundi la nchi nane walishiriki kwenye karamu iliyoandaliwa tarehe 6 mwezi Juni usiku kwenye mji mdogo wa Heiligendamm ulioko katika pwani ya mashariki ya Ujerumani kwa ajili ya kufungua rasmi mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane mwaka huu.
  • Umoja wa mataifa wataka nchi mbalimbali kujenga kinga dhidi ya ongezeko la joto la dunia
  •  2007/06/06
    Tarehe 5 mwezi Juni ni siku ya mazingira duniani, ambapo Umoja wa Mataifa uliitisha mkutano wa kimataifa wa upunguzaji maafa huko Geneva na kujadili hali mpya ya kukabili na kupunguza maafa katika mazingira ya kuongezeka kwa joto duniani, pamoja na hatua zenye ufanisi zinazochukuliwa kukabili changamoto hiyo.
  • Nchi zinazoendelea zajitahidi kuhifadhi mazingira safi
  •  2007/06/05
    Tarehe 5 Juni ni maadhimisho ya mwaka wa 36 wa "siku ya mazingira safi duniani". Miaka ya karibuni, kutokana na matatizo ya mazingira yanavyozidi kuzingatiwa, nchi zinazoendelea zinachukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira duniani.
  • Bush atakabiliwa na masuala mbalimbali katika ziara barani Ulaya
  •  2007/06/04
    Rais George W. Bush wa Marekani tarehe 4 Juni atakwenda Ulaya kufanya ziara ya siku 8, ambapo pamoja na kuhudhuria mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8 za viwanda utakaofanyika nchini Ujerumani, pia atazizuru nchi tano za Czech, Poland, Italia, Albania na Bulgaria.
  • Tony Blair afanya ziara ya mwisho barani Afrika
  •  2007/06/01
    Tarehe 31 Mei waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair alifika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ambapo ni kituo chake cha mwisho katika ziara yake barani Afrika na pia ni ziara yake ya mwisho katika nchi za nje. Vyombo vya habari vinasema hii ni "safari ya kuaga", na wachambuzi wanaona sababu ya Bw. Blair kuchagua Afrika kufanya ziara yake ya kuaga ni kutaka kutukuza sera zake kuhusu Afrika baada ya sera zake kuhusu Iraq kushindwa.
  • Baraza la usalama lapitisha azimio la kuunda mahakama ya kimataifa kuhusu mauaji ya Rafik Hariri
  •  2007/05/31
    Tarehe 30 mwezi Mei, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio No. 1757 kwa kura 10 za ndiyo, ambapo kura 5 hazikupigwa, likiamua kuunda mahakama maalumu ya kimatiafa kushughulikia kesi ya mauaji ya Rafik Hariri aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon
  • Uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi kati ya Asia na Ulaya waendelea kuimarika
  •  2007/05/30
    Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje, wa Asia na Umoja wa Ulaya, ulimalizika tarehe 29 huko Hamburg, nchini Ujerumani. Mkutano huo umeonesha nia ya pande mbili, Asia na Ulaya, kutaka kuimarisha ushirikiano kati yao, ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja.
  • China na nchi za Umoja wa Ulaya zaanzisha uhusiano wa kimkakati na wa kiwenzi kwa pande zote
  •  2007/05/29
    Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Asia na Ulaya tarehe 28 ulimalizika katika mji wa bandari Hamburg, kaskazini mwa Ujerumani. Mapema katika siku hiyo waziri mpya wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi alikutana na mawaziri wa nchi tatu muhimu za Umoja wa Ulaya
  • China yaimarisha zaidi kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma
  •  2007/05/29
    Ofisa wa wizara ya afya ya China tarehe 29 hapa Beijing amesema, serikali ya China inafanya juhudi kutekeleza "Mkataba wa udhibiti wa tumbaku", na imeanza kurekebisha "Vifungu vya usimamizi wa hali ya afya ya sehemu za umma", baada ya marekebisho hayo, China itaimarisha zaidi kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye sehemu za umma.
  • Ikulu ya Marekani yaanza kufikiria sera mpya kuhusu Iraq
  •  2007/05/28
    Ingawa mpango wa Marekani wa kuongeza askari elfu 30 katika nchi ya Iraq bado haujatimizwa, lakini rais Bush na wasaidizi wake wameonesha kuwa, sasa wanaanza kufikiria sera mpya kuhusu Iraq, baada ya kumaliza kuongeza askari nchini humo, na umuhimu wa sera hizo ni kupunguza idadi ya askari wa Marekani nchini Iraq
  • Jeshi la Israel lawakamata maofisa wengi wa Hamas
  •  2007/05/25
    Jeshi la ulinzi la Israel alfajiri ya tarehe 24 liliwakamata maofisa 33 wa kundi la Hamas kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Jordan, kati ya maofisa hao alikuwapo waziri mmoja. Sambamba na hayo, migogoro ya kisilaha kati ya jeshi la Israel na vikundi vyenye silaha vya Palestina inaendelea kwenye sehemu ya Gaza, pande zote mbili zinakataa kusimamisha vita, mapambano ya kutumia silaha kati ya Palestina na Israel yatakuwa makali.
  • Soko la pamoja la mashariki na kusini mwa Afrika lapiga hatua za maendeleo kwenye utandawazi wa uchumi.
  •  2007/05/24
    Wasikilizaji wapendwa, mkutano wa 12 wa wakuu wa nchi wa soko la pamoja la mashariki na kusini mwa Afrika, ulifungwa tarehe 23 huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Mkutano huo ulipitisha mpango wa kuanzisha umoja wa ushuru wa forodha wa mashariki na kusini mwa Afrika kabla ya mwishoni mwa mwaka 2008, hatua ambayo inaonesha umoja huo wa uchumi wa kikanda, ambao unachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa barani Afrika, umepiga hatua moja kwa kuelekea katika lengo la utandawazi wa uchumi wa kanda hiyo.
  • Mazungumzo ya pili ya uchumi wa kimkakati kati ya China na Marekani yapata mafanikio.
  •  2007/05/24
    Mazungumzo ya pili ya uchumi wa kimkakati kati ya China na Marekani yamemalizika tarehe 23 Mei huko Washington. Katika mazungumzo hayo ya siku mbili, pande hizo mbili zilibadilishana maoni kuhusu huduma za fedha, nishati na uhifadhi wa mazingira, na ongezeko la uwiano la uchumi, na zilifikia maoni mengi ya pamoja.
  • Harakati za kupanda miti bilioni 1 duniani zapata mafanikio ya mwanzo
  •  2007/05/23

    Tarehe 22 Mei mwaka huu ilikuwa ni siku ya aina nyingi za viumbe duniani. Siku hiyo Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu yake yaliyopo mjini Nairobi, Kenya lilisema, tangu harakati za kupanda miti bilioni 1 ianzishwe na Umoja wa Mataifa mwaka jana, idadi ya miti ambayo pande mbalimbali ziliahidi kuipanda kote duniani imezidi bilioni 1. Habari hiyo inawatia moyo watu na kuvutia ufuatiliaji wa watu kuhusu suala la kuhifadhi mazingira.

  • Wateja wa Marekani wapenda "Made in China"
  •  2007/05/22

    Mmarekani Mike, ambaye ni mkazi wa Washington, wiki iliyopita alinunua kofia moja. Bw. Mike anaipenda sana kofia hiyo, si kwa kuwa bei yake ni rahisi tu, bali ni kofia iliyotengenezwa vizuri na kusifiwa na watu wengi. Watu wengine kutoka katika familia yake walitaka pia kununua kofia kama yake, baada ya kuangalia nembo yake, na kugundua kumbe kofia hiyo ilitengenezwa nchini China! "Made in China" siyo kitu kigeni kwa wamarekani, maneno hayo yameingia majumbani kwa watu wa Marekani, vitu vilivyozalishwa nchini China vimewanufaisha kihalisi.

  • Spika Wu Bangguo aeleza kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya makampuni ya China na Afrika
  •  2007/05/22
    Spika wa bunge la umma la China Bwana Wu Bangguo ambaye yuko ziarani nchini Misri tarehe 21 alihudhuria mkutano wa ushirikiano kati ya makampuni ya China na Afrika uliofanyika huko Cairo. Kwenye mkutano huo spika Wu Bangguo alitoa hotuba iitwayo "Tuandike kwa pamoja ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya China na Afrika".
  • Ushirikiano kati ya China na Misri katika sekta ya usafiri wa ndege una mustakabali mzuri
  •  2007/05/21
    Spika wa bunge la umma la China Bwana Wu Bangguo ambaye yuko ziarani nchini Misri tarehe 20 alipotembelea kiwanda cha kutengeneza ndege aina ya K-8E kilichoko sehemu ya kusini ya Cairo, alitumai kuimarisha ushirikiano kati ya China na Misri katika sekta ya usafiri wa ndege.
  • Bw Blair na Rais Bush wakutana na kusisitiza uhusiano wa washirika kati ya Uingereza na Marekani
  •  2007/05/18
    Rais George W. Bush wa Marekani tarehe 17 Mei alikuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair kwenye Ikulu ya Marekani, ambapo wamesisitiza uhusiano wa ushirika kati ya Marekani na Uingereza, na kutetea sera ya nchi hizo mbili kuhusu Iraq.
  • Mapambano kati ya magaidi na serikali kabla ya uchaguzi wa bunge nchini Algeria
  •  2007/05/17
    Uchaguzi wa bunge la Algeria unafanyika tarehe 17 mwezi wa Mei, lakini tarehe 16, siku moja kabla ya uchaguzi huo, mlipuko ulitokea mjini Constantine, mashariki mwa Algeria, polisi mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa
  • Mkutano wa afya duniani lapinga kwa mara ya 11 pendekezo kuhusu suala la Taiwan
  •  2007/05/15
    Mkutano wa 60 wa afya duniani ulifunguliwa tarehe 14 Asubuhi kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva barani Ulaya, na pendekezo lililotolewa na nchi chache kuhusu kuiruhusu Taiwan kuwa nchi mwanachama wa Shirika la afya duniani WHO siku hiyo lilikataliwa kwenye mkutano huo, na pendekezo hilo halijawekwa kwenye ajenda ya muda ya mkutano huo, na hii ni mara ya 11 kwa mkutano huo kukataa pendekezo kuhusu suala la Taiwan.
  • Wajenzi wa mradi wa kuzalishaji umeme wa China nchini Sudan
  •  2007/05/14
    Kwenye jangwa lililoko kaskazini mwa Khartoum, mji mkuu wa Sudan, watu wanaweza kuona minara mirefu ya chuma ya rangi ya fedha, minara hiyo ya nyaya za umeme ni ya mfumo mpya wa umeme kwenye sehemu ya kaskazini mwa Sudan, ambao unajengwa na wahandisi wa kampuni ya mradi wa kuzalisha umeme ya mji wa Harbin wa China.
  • Boma la Marwi-ushahidi mkubwa wa urafiki kati ya China na Sudan
  •  2007/05/11
    Boma la Marwi lililoko kwenye sehemu ya kaskazini ya Sudan, ni kituo kikubwa cha pili cha kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji kilichojengwa kwenye mto Nile baada ya Boma la Aswan nchini Misri, pia ni mradi mkubwa kabisa wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji nchini Sudan hata barani Afrika. Boma hilo linachukuliwa kuwa ni mfano mpya wa urafiki kati ya China na Sudan. Tarehe 20 mwezi Mei mwaka 2003.
  • Barabara zilizojengwa na Wachina zimeimarisha urafiki kati ya watu wa China na nchi za Afrika
  •  2007/05/10
    Katika mji wa Addis Ababa, Ethiopia kuna barabara ya urafiki ya Ethiopia na China inayojulikana kwa wakazi wote wa mji huo. Miaka mitatu iliyopita, kampuni ya barabara na daraja ya China ilikamilisha ujenzi wa barabara hiyo yenye sifa bora katika muda mfupi, ambapo kampuni hiyo ya China ilisifiwa sana nchini humo.
  • Kampuni ya Huawei ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya China na Misri
  •  2007/05/09
    Kampuni ya Huawei ni kampuni kubwa ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya habari nchini China, kampuni hiyo ni mfano mzuri wa ushirikiano kati China na Misri. Mwaka 1999 kampuni ya Huawei ilianzisha tawi lake nchini Misri, katika miaka minane iliyopita kampuni hiyo ilipata maendeleo makubwa katika kutoa huduma ya vifaa vya mawasiliano ya habari nchini Misri, kufunga vifaa hivyo na mtandao mkubwa wa internet.
  • Kwanini Bwana Sarkozy ameweza kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu nchini Ufaransa?
  •  2007/05/07
    Katika duru la pili la upigaji kura wa uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Ufaransa, mgombea wa rais wa chama cha muungano wa harakati za umma cha mrengo wa kulia cha Ufaransa Bw Nicolas Sarkozy alimshinda mgombea mwingine Bibi Segolene Royal wa chama cha jamii cha mrengo wa kushoto cha Ufaransa, na kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ufaransa, ushindi wake unatokana na sababu mbalimbali.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44