Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Bw. Liu Guijin azungumzia ziara yake nchini Sudan
  •  2008/02/28
    Mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia Suala la Darfur Bw. Liu Guijin, tarehe 27 huko Khartoum aliitisha mkutano na waandishi wa habari, akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ziara yake nchini Sudan. Bw. Liu Guijin alifanya ziara ya siku nne nchini Sudan kuanzia tarehe 24 hadi 27.
  • Kundi la okestra la New York lafanya maonesho ya kihistoria mjini Pyongyang
  •  2008/02/27
    Kundi maarufu la muziki la Marekani yaani Kundi la Okestra la New York, tarehe 26 lilifanya maonesho ya kihistoria mjini Pyongyang, mji mkuu wa Korea ya Kaskazini. Hii ni mara ya kwanza kwa kundi la muziki la Marekani kufanya ziara nchini Korea ya Kaskazini tokea nchi hiyo iasisiwe Septemba 1948. Maonesho yamepata mafanikio makubwa.
  • Je, uchumi wa Marekani unaokabiliwa na hatari ya kuzorota utaathiri ongezeko la uchumi duniani?
  •  2008/02/26
    Tokea mwezi Aprili mwaka jana msukosuko wa mikopo ya nyumba ulipotokea nchini Marekani, uchumi wa Marekani umekuwa katika hali ya kusuasua.
  • Waziri wa mambo ya nje wa Sudan aeleza uhusiano kati ya Sudan na China
  •  2008/02/25
    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Bw. Deng Alor tarehe 24 huko Khartoum alikuwa na mazungumzo na mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia suala la Darfur Bw. Liu Guijin, aliyekwenda ziarani nchini Sudan. Baada ya mazungumzo yao, waziri Deng Alor alihojiwa na waandishi wa habari wa China.
  • Mjumbe maalumu wa serikali ya China azungumzia suala la Darfur
  •  2008/02/22
    Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia suala la Darfur Bw. Liu Guijin, tarehe 21 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini London, alifahamisha hali ilivyo ya mgogoro wa Darfur na msimamo wa serikali ya China kuhusu suala hilo.
  • Kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ni kazi ya pamoja duniani
  •  2008/02/21
    Kongamano la Tano la watungaji sheria la kundi la nchi 8 na nyingine tano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani lilifunguliwa tarehe 20 mjini Brasilia, mji mkuu wa Brazil. Mjumbe wa China aliyehudhuria kongmanano hilo alisema, ni lazima suala hili litekelezwe kwa busara
  • Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa Pakistan yatangazwa
  •  2008/02/20
    Kazi ya kuhesabu kura kwenye uchaguzi wa bunge la Pakistan iliyofanyika tarehe 19 inaonesha kuwa, Chama cha Umma cha Pakistan kimepata kura nyingi zaidi, lakini kutokana na kuwa kura hizo hazikuzidi nusu ya kura zote, chama hicho hakiwezi kuunda serikali peke yake
  • Suala la Kosovo lautatiza Umoja wa Ulaya
  •  2008/02/19
    Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya ulifanyika tarehe 18 mjini Brussels kujadili msimamo wa pamoja kuhusu suala la Kosovo baada ya kujitangazia uhuru. Lakini kutokana na tofauti ambazo ni vigumu kuzisawazisha, mwishowe mkutano huo ulipaswa kukubali kila nchi mwanachama ifanye uamuzi wake yenyewe kuhusu kutambua uhuru wa Kosovo.
  • Kosovo yajitangazia uhuru kwa upande mmoja
  •  2008/02/18
    Bunge la Kosovo tarehe 17 lilifanya mkutano maalumu na kupitisha taarifa ya kujitangazia uhuru, kwa upande mmoja imejitangazia uhuru na kujitenga na Serbia. Taarifa inasema, Kosovo itatekeleza mpango wa mjumbe maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Marti Ahtisari kuhusu "uhuru wa Kosovo chini ya usimamizi wa kimataifa", na kukubali Umoja wa Ulaya kutuma kundi maalum kuingia Kosovo na kutaka jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa liendelee kuwepo ndani ya Kosovo.
  • Ni vigumu kwa Lebanon kuondokana na hali ngumu ya kisiasa
  •  2008/02/15
    Waungaji mkono elfu kumi kadhaa wa serikali ya Lebanon tarehe 14 walifanya mkutano wa hadhara kwenye katika uwanja wa mashujaa waliouawa huko Beirut, ili kumkumbuka waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafik al-Hariri aliyeuawa miaka mitatu iliyopita
  • Rais Bush wa Marekani kufanya ziara katika nchi tano za Afrika
  •  2008/02/14
    Rais George Bush wa Marekani anatazamiwa kufanya ziara katika nchi tano za Afrika Benin, Tanzania, Rwanda, Ghana na Liberia kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 21 mwezi huu. Wakati wa ziara yake hiyo, rais Bush atafanya mazungumzo na viongozi wa nchi hizo za Afrika kuhusu kuhimiza mageuzi ya demokrasia, biashara huria na kuharakisha maendeleo ya uchumi wa Bara la Afrika
  • Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Pakistan asifu maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing
  •  2008/02/13
    Pakistan ni nchi jirani mwema wa China, licha ya kuwa nchi hizo mbili zina uhusiano mzuri wa kisiasa na kiuchumi, pia zina ushirikiano mkubwa katika mambo ya michezo. Kadiri michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008 inavyokaribia, ndivyo Pakistan inavyozidi kufuatilia hali ya maandalizi ya michezo hiyo
  • Hali ya Chad imekuwa tulivu kwa sasa
  •  2008/02/05
    Baada ya mapambano ya siku mbili, tarehe 4 hali ya N'djamena mji mkuu wa Chad ilirudi kuwa ya utulivu. Vikosi vya upinzani havikufanya mashambulizi tena baada ya kuondoka mjini humo alasiri tarehe 3. Jioni ya tarehe hiyo serikali ya Chad ilitangaza kwamba imekomesha jaribio la uasi
  • Nani anaweza kuiokoa Kenya?
  •  2008/02/04
    Ingawa vyama viwili vya Kenya vilisaini Mpango wa Amani tarehe 1 Februari usiku, lakini hali ya nchi hiyo bado si tulivu. Jumuiya ya kimataifa inatiwa wasiwasi tena kuhusu hali inavyoendelea nchini humo.
  • Hatma ya Chad itakuwaje?
  •  2008/02/04
    Tarehe 3 mapambano makali kati ya jeshi la serikali na vikosi vya upinzani yaliendelea huko N'Djamena, mji mkuu wa Chad, na huku vikosi vingine vikifanya mashambulizi dhidi ya jeshi la serikali kwenye sehemu ya mpaka wa mashariki wa nchi hiyo. Mpaka sasa haijulikani mapambano hayo yataendelea vipi.
  • Suala la Kenya ni ajenda muhimu kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika
  •  2008/02/01
    Mkutano wa 10 wa viongozi wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika ulifunguliwa tarehe 31 Januari mjini Addis Ababa, mada ya mkutano huo ni "Maendeleo ya viwanda barani Afrika", viongozi au wajumbe kutoka nchi 53 za Umoja wa Afrika watajadiliana kuhusu maendeleo ya viwanda barani humo, uchaguzi wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika, msukosuko wa kisiasa nchini Kenya na kuunda serikali ya muungano wa nchi za Afrika.
  • Marekani haijabadili msimamo wake kuhusu suala la hali ya hewa
  •  2008/01/31
    Tarehe 30 Januari mkutano wa kujadili usalama wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa uliohudhuriwa na nchi na makundi makubwa ya kiuchumi ulifanyika huko Hawaii. Hii ni mara ya pili kwa Marekani kuitisha mkutano wa namna hii, ambapo wajumbe kutoka nchi 16, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa walihudhuria mkutano huo.
  • Mazungumzo kati ya serikali ya Kenya na upande wa upinzani yaanza
  •  2008/01/30
    Kutokana na usuluhishi wa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan, mazungumzo kati ya chama tawala kinachoongozwa na rais Mwai Kibaki wa Kenya PNU, na chama cha upinzani cha ODM kinachoongozwa na Bw. Raila Odinga yalianza rasmi tarehe 29 alasiri huko Nairobi.
  • Ziara ya Pervez Musharraf barani Ulaya yapata mafanikio kwa kiasi fulani
  •  2008/01/29
    Tarehe 28 Rais Pervez Musharraf wa Pakistan alimaliza ziara yake ya siku nane barani Ulaya. Vyombo vya habari vinaona kuwa lengo kuu la ziara ya rais huyo barani humo ni kuboresha sura ya Pakistan duniani, na kuondoa kutoelewana na kutafuta imani na uungaji mkono kutoka kwa nchi za Ulaya. Lakini kwa kuzingatia matokeo ya ziara yake, rais Pervez Musharraf amefanikiwa kwa kiasi fulani.
  • Ushirikiano wa nchi mbalimbali waleta mustakabali mzuri duniani
  •  2008/01/28
    Mkutano wa mwaka 2008 wa Baraza la uchumi la dunia ulifungwa tarehe 27 huko Davos, nchini Uswisi. Masuala yaliyozungumzwa sana kwenye mkutano huo wa siku 5 yalikuwa ni pamoja na uchumi wa dunia, maendeleo endelevu na mazungumzo ya raundi ya Doha.
  • Marekani yatangaza mpango wa kuhimiza mambo ya uchumi
  •  2008/01/25
    Serikali ya Marekani na bunge la nchi hiyo tarehe 24 zilifikia makubaliano kuhusu mpango wa kuhimiza mambo ya uchumi. Kutokana na mpango huo serikali ya Marekani itarudisha kodi yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100 kwa zaidi ya familia milioni 100 za Marekani, ili kuhamasisha watu kufanya matumizi, na kuzuia uchumi wa Marekani usididimie, kwani uchumi wa nchi hiyo sasa uko katika hali ya kudidimia.
  • Waziri wa mambo ya nje wa Russia aeleza sera ya kidiplomasia ya Russia
  •  2008/01/24
    Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov tarehe 23 mwezi Januari huko Moscow kwenye mkutano na waandishi wa habari aliwaeleza mafanikio iliyoyapata Russia katika shughuli za kidiplomasia mwaka 2007, na sera ya kidiplomasia ya nchi hiyo.
  • Suala la nyukilia la Iran lawa na utatanishi zaidi
  •  2008/01/23
    Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 6 kuhusu suala la nyukilia la Iran, ulimalizika tarehe 22 mwezi Januari huko Berlin. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Frank Walter Steinmeier, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya mkutano huo alisema, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa suala la nyukilia la Iran
  • Migogoro yazikabili Palestina na Israel
  •  2008/01/22
    Katika siku nne zilizopita, sehemu ya Palestina na Israel imekumbwa tena na hali ya wasiwasi, kwani Israel imeanza kuweka vikwazo kwa pande zote dhidi ya ukanda wa Gaza ili kuwalazimisha watu wenye silaha wa Palestina kuacha kurusha maroketi dhidi ya sehemu ya kusini ya Israel, na wakazi wa huko wamekabiliwa na maisha magumu zaidi.
  • Kwa nini waziri mkuu wa Japan Yasuo Fukuda atilia mkazo sera ya "mazingira " ?
  •  2008/01/21
    Tarehe 21 hali ya "vuta nikuvute" itatokea katika bunge la Japan. Wakati huo waziri mkuu wa Japan Bw. Yasuo Fukuda alikuwa anaulizwa maswali na wabunge kuhusu sera zake alizotoa tarehe 18. Kwenye hotuba aliyotoa tarehe 18 alitangaza na kutilia mkazo sera tano za kitaifa
  • Kwa nini nchi za Ghuba zajitahidi kuisogelea karibu Iran?
  •  2008/01/18
    Hivi karibuni Rais George Bush alipokuwa ziarani kwenye nchi za Ghuba alijitahidi kutangaza fikra yake kuhusu "tishio la Iran" ili kuitenga zaidi Iran. Lakini alipoondoka tu nchi za Ghuba zikatangaza kuwa zitaendelea kuimarisha uhusiano na Iran.
  • Ziara ya Rais Gorge Bush kwenye nchi za Mashariki ya Kati imepata mafanikio gani?
  •  2008/01/17
    Tarehe 16 Rais George Bush alimaliza ziara yake kwenye nchi za Mashariki ya Kati. Kwenye ziara hiyo Rais Bush alizitembelea Israel, Palestina, Kuwait, Bahrain, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Misri. Mapema kabla ya ziara yake, Rais Gorge Bush alisema wazi kwamba ziara yake ina malengo mawili, moja ni kusukuma mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel, nyingine ni kuziunganisha nchi za Kiarabu ili kudhibiti Iran. Lakini je ziara yake imefikia malengo hayo?
  • Ziara ya Bw Bush kwenye sehemu ya ghuba yaonesha mvutano mkali
  •  2008/01/16
    Rais George Bush wa Marekani tarehe 16 mwezi Januari alimaliza ziara yake ya siku 8 kwenye sehemu ya mashariki ya kati, na alirudi nchini Marekani kutoka Misri. Katika ziara hiyo rais Bush alitumia muda mwingi kutembelea nchi nne za Kuwait, Bahrain, Umoja wa falme za kiarabu na Saudi Arabia, "Iran ni tishio kubwa dhidi ya usalama wa sehemu ya ghuba" yalikuwa ni maneno aliyoyasema mara kwa mara katika ziara hiyo.
  • Palestina na Israel zafanya mazungumzo kuhusu masuala ya msingi
  •  2008/01/15
    Waziri wa mambo ya nje wa Israel Bi. Tzipi Livni na waziri mkuu wa zamani wa Palestina Bw. Ahmed Qureia tarehe 14 walifanya mazungumzo huko Jerusalem kuhusu masuala ya msingi yakiwemo hatma ya Jerusalem, kurudishwa kwa wakimbizi wa Palestina na mpaka wa Palestina baada ya kuwa nchi. Mazungumzo hayo kwa mara ya kwanza yaligusia masuala hayo ya msingi tokea mazungumzo yalipoanza tena mwezi Desemba mwaka uliopita.
  • Suluhisho la suala la nyuklia la Iran limekaribia?
  •  2008/01/14
    Makamu wa rais wa Iran ambaye pia ni mwenyekiti wa shirika la nishati ya atomiki ya nchi hiyo Bw. Gholam Reza Aghazadeh alisema, Iran inapenda kutatua masuala yote yaliyobaki kuhusu mpango wake wa nyuklia mwezi Februari mwaka huu.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44