Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Balozi mpya wa Marekani nchini Iraq hatafanikiwa chochote
  •  2007/03/30
    Balozi mpya wa Marekani nchini Iraq Bw. Ryan Crocker tarehe 29 aliapishwa chini ya ulinzi mkali mjini Baghdad. Katika siku hiyo hiyo katika sehemu ya Khalis, kaskazini ya Baghdad, ilitokea milipuko mingi na kusababisha vifo vya watu 107 na wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa.
  • Umoja wa Nchi za Kiarabu waahidi kutatua migogoro ya kikanda kwa njia ya kidiplomasia
  •  2007/03/29
    Mkutano wa 19 wa siku mbili wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Nchi za Kiarabu unaofanyika kwa siku mbili ulianza tarehe 28 mwezi Machi huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, viongozi wa nchi za kiarabu wanaoshiriki kwenye mkutano huo wameahidi kutatua migogoro ya sehemu ya mashariki ya kati kwa njia ya kidiplomasia.
  • Marais wa China na Russia wazindua "Maonesho ya mwaka wa China"
  •  2007/03/28
    "Maonesho ya mwaka wa China", ambayo ni maonesho ya kitaifa yanayochukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa ya China yanayooneshwa katika nchi za nje kuhusu mambo ya maeneo mengi ya China. Maonesho hayo yalizinduliwa tarehe 27 mwezi Machi nchini Russia na rais Hu Jintao, ambaye hivi sasa anafanya ziara nchini Russia pamoja na rais Putin wa Russia.
  • Jeshi la Marekani laonesha nguvu yake katika Ghuba ya Uajemi ili kuishinikiza Iran
  •  2007/03/28
    Kuanzia tarehe 27 jeshi la baharini la Marekani lilianza kufanya luteka katika Ghuba ya Uajemi. Hiyo ni luteka kabambe kabisa katika Ghuba hiyo tokea vita vya Iraq zianze mwaka 2003. Kutokana na kuwa mazoezi hayo yanafanyika katika wakati nyeti ambapo Iran imewakamata askari wa Uingereza na pande mbili kati ya Iran na Uingereza haziafikiani, luteka hiyo inafuatiliwa sana.
  • Marais wa China na Russia wazindua "Mwaka wa China"
  •  2007/03/27
    Sherehe ya kuzindua "Mwaka wa China" wa Russia ilifanyika usiku wa tarehe 26 mwezi Machi kwenye ukumbi wa ikulu ya Russia mjini Moscow. Rais wa China Hu Jintao anayefanya ziara nchini Russia na rais Putin wa Russia walishiriki sherehe ya uzinduzi.
  • Waziri mkuu wa Japan aomba msamaha kuhusu suala la "wanawake wa kustarehesha"
  •  2007/03/27
    Tarehe 26 Machi kutokana na shinikizo la ndani na nchi za nje waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe aliomba rasmi msamaha kuhusu suala la wanawake waliolazimishwa kuwastarehesha askari wa Japan katika vita vya pili vya dunia.
  • Ban Ki-moon na Rice watembelea Palestina na Israel kwa wakati mmoja kuhimiza mazungumzo ya amani
  •  2007/03/26
    Tarehe 25 katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice walioko ziarani kwenye sehemu ya mashariki ya kati kwa mbalimbali walitembelea Palestina, na kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel.
  • Hu Jintao ahojiwa na vyombo vya habari vya Russia kabla ya kufanya ziara nchini Russia
  •  2007/03/26
    Rais Hu Jintao atafanya ziara ya kiserikali nchini Russia kuanzia tarehe 26 hadi 28 mwezi Machi, na kushiriki kwenye sherehe ya kuzindua "mwaka wa China". Kabla ya ziara yake rais Hu Jintao alihojiwa na waandishi habari wa vyombo 6 vya habari vya Russia hapa Beijing likiwemo shirika la habari la Interfax.
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa afanya ziara ya ghafla mjini Baghdad
  •  2007/03/23
    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 22 aliwasili ghafla mjini Baghdad kwa ziara ya siku moja nchini Iraq. Hii ni mara ya kwanza kwa katibu mkuu huyo kuitembelea Iraq.
  • Hali ya usalama nchini Somalia yazidi kuwa mbaya siku hadi siku
  •  2007/03/22
    Mapambano ya kisilaha yalitokea tarehe 21 huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na kusababisha vifo na majeruhi 17. Hayo ni mapambano makali kabisa kutokea jeshi la kundi la mahakama za kiislamu la Somalia lishindwe na kukimbia mji wa Mogadishu. Mapambano hayo yamefanya hali mbaya ya usalama nchini Somalia kuwa mbaya zaidi.
  • Israel yafanya mazoezi ya kitaifa ya kujikinga dhidi ya mashambulizi ya kigaidi
  •  2007/03/21
    Tarehe 20 saa nane mchana katika miji mikubwa nchini Israel, kutokana na milio ya king'ora mazoezi ya kujikinga dhidi ya mashambulizi ya kigaidi yalianza katika miji hiyo. Mazoezi hayo yalifanyika kwa siku mbili, polisi, askari wa jeshi, wazimamoto na waokoaji wa dharura walishiriki kwenye mazoezi hayo.
  • Watu wa Iraq wana hamu ya kuishi kwa utulivu
  •  2007/03/19
    Jeshi la muungano la Marekani na Uingereza lilianzisha vita vya Iraq tarehe 20 Machi mwaka 2003, kwa lengo la kupindua utawala wa Saddam Hussein. Sasa ni miaka minne imepita, vita hivyo vimemalizika lakini askari wa Marekani na Uingereza bado wako nchini Iraq na mapambano ya kimabavu yanaendelea kutokea mara kwa mara nchini humo
  • Baraza jipya la mawaziri la serikali mpya ya Palestina laundwa
  •  2007/03/16
    Tarehe 15 pande mbalimbali za Palestina zilikubaliana kuhusu orodha ya baraza la mawaziri la serikali mpya ya Palestina. Siku hiyo waziri mkuu wa serikali ya Palestina Bw. Ismail Haniyeh alikabidhi orodha hiyo kwa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas, na Bw. Abbas aliikubali orodha hiyo.
  • Utatuzi wa suala la nyuklia umekuwa ni ushirikiano mzuri kati ya Korea ya Kaskazini na Marekani
  •  2007/03/15
    Mkurugenzi mkuu wa Baraza la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohammed El Baradei tarehe 14 alimaliza ziara yake nchini Korea ya Kaskazini, baada ya ziara hiyo alisema Korea ya Kaskazini imekubali kurudi tena kwenye baraza hilo.
  • Hali ya usalama mjini Mogadishu bado ni mbaya
  •  2007/03/14
    Tarehe 13 mashambulizi ya mabomu yalitokea mjini Mogadishu kwa lengo la kumuua rais Yusufu wa serikali ya mpito ya Somalia. Ingawa rais Yusuf aliponea chupuchupu, lakini kutokana na kuwa tukio hilo lilitokea tu baada ya bunge la Somalia kuamua kuhamisha serikali ya mpito mjini Mogadishu, watu wanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa mji huo.
  • Baraza la haki za binadamu lafanya mkutano wa kwanza mwaka huu
  •  2007/03/13
    Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 12 lilifanya mkutano wa kwanza katika makao yake makuu mjini Geneva.
  • Manowari za China zashiriki kwenye luteka ya nchi nyingi
  •  2007/03/12
    Wasikilizaji wapendwa, manowari za nchi nane zilifanya luteka inayojulikana kama "Amani--07" kwenye sehemu ya kaskazini mwa bahari ya Uarabuni karibu na Pakistan. Manowari za jeshi la ukombozi la umma la China zilishiriki kwenye luteka hiyo na kuhitimisha aina mbalimbali za shughuli za luteka hiyo.
  • Wanawake wa Palestina wajitahidi kujiendeleza katika mazingira magumu
  •  2007/03/08
    Tarehe 8 Machi, siku ya wanawake duniani, wanawake wa kila pembe duniani wanafanya shughuli mbalimbali kusherehekea siku hiyo.
  • Mkutano wa nchi za Asia ya Kusini Mashariki dhidi ya ugaidi wasisitiza ushirikiano
  •  2007/03/07
    Mkutano wa siku mbili wa nchi za Asia ya Kusini Mashariki kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi ulimalizika tarehe 6 mjini Jakarta. Wajumbe kutoka nchi sita za kanda hiyo kwa kauli moja waliona kuwa kuimarisha ushirikiano ni muhimu zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi, na ni njia pekee ya kuhakikisha usalama wa kanda hiyo.
  • Vikwazo vya mazungumzo ya duru la Duha havitaondolewa katika muda mfupi
  •  2007/03/06
    Katibu mkuu wa WTO Bw. Pascal Lamy tarehe 5 huko Geneva alifanya mazungumzo na wajumbe wa nchi muhimu wanachama wa WTO Marekani, Umoja wa Ulaya na India. Baada ya mazungumzo hayo mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya biashara Bw. Peter Mandelson alisema, Umoja wa Ulaya unashikilia msimamo ule ule wa zamani kuhusu biashara ya mazao ya kilimo
  • Mazungumzo ya duru la Doha yaingia katika kipindi muhimu
  •  2007/03/05
    Nchi wanachama kadhaa muhimu wa shirika la biashara duniani, WTO zikiwemo Marekani, Umoja wa Ulaya, Brazil na India zimeamua kufanya mazungumzo tarehe 5 mwezi Machi huko Geneva pamoja na Katibu mkuu wa WTO Bw. Pascal Lamy
  • Mwaka wa kimataifa wa shughuli za uchunguzi kwenye ncha za dunia wazinduliwa Paris
  •  2007/03/02
    Tarehe mosi Machi mwaka wa kimataifa wa shughuli za uchunguzi kwenye ncha mbili za dunia kuanzia mwaka 2007 hadi 2008 ulizinduliwa huko Paris. Hizi ni shughuli ambazo zitazingatia zaidi uhusiano kati ya uchafuzi wa hewa uliosababisha kuongezeka kwa joto duniani na ncha mbili za dunia. Wanasayansi elfu 50 kutoka nchi 63 watashiriki kwenye shughuli hizo.
  • Mkutano wa amani kuhusu suala la Iraq wafuatiliwa na watu
  •  2007/03/01
    Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw. Hoshyar Zebari, tarehe 28 mwezi Februali huko Baghdad alisema, Iran na Syria zimekubali kushiriki kwenye mkutano wa amani utakaofanyika hivi karibuni, wenye lengo la kuhimiza Iraq kuwa na utulivu. Siku hiyo taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Syria ilithibitisha kuwa Syria itatuma mwakilishi kuhudhuria mkutano huo.
  • Mtaalamu wa China azungumzia ziara ya Cheney katika nchi za Asia na Pasifiki
  •  2007/02/28
    Makamu wa rais wa Marekani Bwana Dick Cheney katika muongo wa tatu wa mwezi Februari alifanya ziara nchini Japan, Australia, Oman, Pakistan na Afghanistan. Naibu mkuu wa taasisi ya uhusiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha umma cha China Bwana Jin Canrong alizungumzia lengo la ziara hiyo na mafanikio aliyopata.
  • Mkutano wa nchi sita wa London wajadili hatua gani zichukuliwe kuhusu suala la nyuklia la Iran
  •  2007/02/27
    Wajumbe wa ngazi ya juu wa nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Marekani, Russia, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani walifanya mkutano tarehe 26 huko London wakijadili ni hatua gani zichukuliwe ili kuhimiza ufumbuzi wa suala la nyuklia la Iran. Mkutano huo ulilenga kusawazisha misimamo ya pande husika mbalimbali kabla ya baraza la usalama kujadili suala la nyuklia la Iran mwanzoni mwa mwezi ujao.
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi saba za Kiislam wataka amani ya mashariki ya kati itimizwe haraka
  •  2007/02/26
    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi saba za Kiislam za Misri, Indonesia, Jordan, Malaysia, Saudi Arabia, Pakistan na Uturuki, pamoja na waziri mkuu wa Pakistan Bwana Shaukat Aziz na katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za Kiislam Bwana Ekmeleddin Ihsanoglu, tarehe 25 walifanya mkutano wa siku moja huko Islamabad, mji mkuu wa Pakistan
  • Suala la nyuklia la Iran litakuwa na mwelekeo gani?
  •  2007/02/23
    Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA Bwana Mohamed El Baradei tarehe 22 alilikabidhi baraza la shirika hilo na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ripoti kuhusu hali ya Iran kutekeleza azimio No. 1737 la baraza la usalama.
  • Bw Tony Blair atangaza kupunguza askari wa Uingereza nchini Iraq
  •  2007/02/22
    Waziri mkuu wa Uingereza Bwana Tony Blair tarehe 21 Februari alitangaza kwenye baraza la chini la bunge la Uingereza kuwa, serikali ya Uingereza imeamua kupunguza idadi ya askari wake nchini Iraq kufikia 5500 kutoka 7100 ya hivi sasa katika miezi kadhaa ijayo
  • Dick Cheney atembelea Japan kutafuta uungaji mkono wa Japan kwa suala la Iraq
  •  2007/02/21
    Makamu wa rais wa Marekani Bwana Dick Cheney tarehe 20 alasiri alifika Tokyo kuanza ziara yake ya siku mbili nchini Japan. Wakati wa ziara yake Bwana Cheney atafanya mazungumzo na viongozi wa Japan kuhusu usalama wa Bara la Asia na mapambano dhidi ya ugaidi kote duniani.
  • Mazungumzo kati ya pande tatu za Marekani, Israel na Palestina hayajapata maendeleo
  •  2007/02/20
    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice ambaye yuko ziarani katika sehemu ya mashariki ya kati, waziri mkuu wa Israel Bw Ehud Olmert na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas tarehe 19 Februari huko Jerusalem walifanya mazungumzo
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44