Jumuiya ya kimataifa yaimarisha udhibiti wa maambukizi ya homa ya mafua ya ndege 2006/02/22 Wataalamu husika wametoa wito wa dharura wakitaka nchi mbalimbali zijitahidi kutokomeza virusi vya homa ya mafua ya ndege vinavyogunduliwa hivi sasa, kufanikisha mapema iwezekanavyo utafiti kuhusu mabadiliko ya virusi vya ugonjwa huo na kutengeneza chanjo yenye ufanisi zaidi.
|
Udhibiti wa maambukizi ya homa ya mafua ya ndege nchini Nigeria wakabiliwa na changamoto kubwa 2006/02/21 Waziri wa habari wa Nigeria Bw. Frank Nweke tarehe 20 huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria alithibitisha kuwa baada ya kugunduliwa homa ya mafua ya ndege ya aina ya H5N1 tarehe 8 mwezi huu kwenye shamba la ufugaji wa kuku kwenye jimbo la Kaduna lililoko kaskazini mwa nchi hiyo.
|
Ni vigumu kwa kundi la Hamas kupita hatua ya kushika hatamu za kiserikali 2006/02/20 Kundi la Hamas la Palestina tarehe 19 limetangaza kumteua rasmi kiongozi wake mmoja Ismail Haniyeh kuwa waziri mkuu mpya wa serikali inayojiendesha ya Palestina.
|
Ushirikiano wa kimataifa ni muhimu katika juhudi za kukinga na kudhibiti homa ya mafua ya ndege 2006/02/17 Majira ya baridi katika sehemu ya kaskazini ya dunia karibu yatapita, lakini homa ya mafua ya ndege haijatoweka, kinyume na hali hiyo ugonjwa huo unaenea kutokana na ndege wanaohama hama
|
Wahandisi watatu wa China wauawa kwa risasi nchini Pakistan 2006/02/16 Wahandisi watatu wa China wameuawa kwa kupigwa risasi kwenye kijiji cha Hub mkoani Baluchistan nchini Pakistan. Rais Pervez Musharraf na waziri mkuu wa Pakistan walilaani vikali tukio hilo na kusema kwamba serikali ya Pakistan itachukua hatua kadiri iwezavyo kuwaadhibu kisheria.
|
Inasemekana kuwa Marekani na Israel zana njama ya kuupindua utawala wa Hamas 2006/02/15 Habari kutoka vyombo vya habari vya Marekani zinasema serikali za Marekani na Israel zimekuwa zikipanga haraka hatua za kuitenga na kuzingira kiuchumi Palestina ili kuulazimisha utawala wa Hamas uporomoke wenyewe.
|
Ni makosa kwa Marekani kutoa ruzuku kwa kampuni zinazouza bidhaa nje 2006/02/14 Kitengo cha utatuzi wa mgogoro cha Shirika la Biashara Duniani, WTO tarehe 13 kilitoa hukumu ikisema, ni makosa ya kukiuka kanuni za WTO kwa Marekani kutoa ruzuku kwa kampuni zake zinazouza bidhaa kwa nchi za nje kwa njia mpya.
|
Lengo la kimkakati la safari ya waziri wa ulinzi wa Marekani katika nchi za Afrika kaskazini 2006/02/13 Waziri wa ulinzi wa Marekani Bwana Donald Rumsfeld tarehe 11 alianza ziara rasmi katika nchi tatu za Afrika kaskazini za Tunisia, Algeria na Morocco.
|
Umoja wa Ulaya wakabiliwa na changamoto ya maambukizi ya homa ya mafua ya ndege 2006/02/13 Maambukizi ya homa ya mafua ya ndege yaliibuka ghafla hivi karibuni kwenye nchi za Ulaya, ambazo zilikuwa na tahadhari kubwa juu ya maradhi hayo.
|
Je, kujengwa kwa kituo cha kimataifa cha kusafisha uranium nchini Russia kutasaidia kutatua suala la nyuklia la Iran? 2006/02/10 Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Russia Sergei Kiriyenko siku chache zilizopita alisema, Russia imeialika Iran kushiriki katika ujenzi wa kituo cha kwanza cha kimataifa cha kusafisha uranium nchini Russia, kutokana na hayo, Iran pengine itakuwa nchi ya kwanza kushiriki katika ujenzi wa kituo hicho.
|
Nchi za Afrika zakabiliwa na changamoto kubwa ya homa ya mafua ya ndege 2006/02/09 Shirika la Afya ya Wanyama Duniani, tarehe 8 lilitoa taarifa ikisema homa ya mafua ya ndege ilizuka katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria.
|
Mkutano kuhusu "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" wafanyika 2006/02/08 Nchi zilizosaini "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" duniani zitakuwa na mkutano wa kwanza kati ya tarehe 6 hadi 17 mwezi Februari huko Geneva.
|
Jumuiya ya kimataifa yazuia kupanuka kwa"mgogoro wa katuni" 2006/02/07 Hivi karibuni waislamu wa nchi nyingi duniani wanaendelea kutoa malalamiko kupinga baadhi ya magazeti ya nchi za Ulaya kuchapisha michoro ya katuni za kumdhalilisha mtume Mohamed wa dini ya kiislamu. Shughuli za kutoa malalamiko zimebadilika kuwa vitendo vya kimabavu
|
Palestina yashughulikia uundaji wa serikali mpya 2006/02/06 Mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmood Abbas tarehe 4 huko Gaza alikuwa na mazungumzo ya kwanza pamoja na viongozi wa kundi la Hamas baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina, na kuwa na majadiliano kuhusu uanzishaji wa serikali mpya ya nchi hiyo.
|
Mabalozi wa nchi za Afrika nchini China wasifu Waraka wa sera za China kwa Afrika 2006/02/03 Serikali ya China hivi karibuni ilitoa rasmi "Waraka wa sera za China kwa Afrika", hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya China kutoa waraka wa sera za China kwa Afrika.
|
Kuthamini utaratibu wa kimataifa wa mikutano ya kupunguza silaha 2006/02/02 katika mkutano wa 1000 wa wajumbe wote wa mazungumzo kuhusu upunguzaji wa silaha uliofanyika tarehe 31 mwezi Januari huko Geneva, kiongozi wa ujumbe wa China Bw. Sha Zukang alifafanua kanuni tatu muhimu za serikali ya China kuhusu shughuli za upunguzaji wa silaha katika siku za baadaye.
|
Umoja wa Mataifa watoa ripoti ikionesha kuwa uchumi wa Afrika utaendelea kuongezeka kwa utulivu 2006/02/01 Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa kuhusu makadirio ya hali ya uchumi duniani katika mwaka 2006 inaonesha kuwa, katika mwaka jana uchumi wa Afrika unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.1, na unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5.5 katika mwaka 2006.
|
Kundi la Hamas lakabiliwa na Mtihani Mpya 2006/01/31 Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Russia ambazo ni pande nne zinazoshiriki katika suala la Mashariki ya Kati, tarehe 30 zimetoa taarifa ikilitaka Kundi la Hamas liitambue Israel na kuacha matumizi ya nguvu.
|
Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani Wafungwa 2006/01/30 Mkutano wa Baraza la Uchumi Duniani umefungwa tarehe 29 huko Davos, Usiwisi. Maendeleo ya uchumi wa China na India na athari zake kwa uchumi wa dunia yalitawala majadiliano yaliyofanyika kwenye mkutano wa mwaka huu wenye kauli mbio isemayo "maendeleo, uvumbuzi na mustakabali".
|
Wataalamu wa China wazungumzia usindi wa Hamas 2006/01/27 Kutokana na hesabu ya kura isiyokamilika ya tarehe 26, kundi la Hamas limeshinda kwenye uchaguzi kwa viti zaidi ya 70 kati ya viti vyote 132 vya bunge.
|
Umoja wa Afrika wajitahidi kutatua wenyewe masuala yake 2006/01/25 Mkutano wa 6 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika, ambao ulifanyika kwa siku 2 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan, ulifungwa tarehe 24. Katika mkutano huo wakuu wa nchi, viongozi wa serikali pamoja na wawakilishi wapatao 36 walishiriki kwenye majadiliano kuhusu masuala ya utamaduni, elimu, ushirikiano kati ya Umoja wa Afrika na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na waliafikiana kwenye nyaraka nyingi.
|
Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika wafuatilia umoja na utulivu wa Afrika 2006/01/24 Mkutano wa 6 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika ulifunguliwa tarehe 23 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan, wawakilishi wa nchi wanachama 53 wakiwemo wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wapatao kiasi cha 30.
|
Uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina 2006/01/23 Uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina umepangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu, huo ni uchaguzi wa pili wa kamati ya kutunga sheria katika muda wa miaka zaidi ya kumi tangu kusainiwa mkataba wa amani wa Oslo na tangu kuasisiwa mamlaka ya taifa ya Palestina.
|
Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika wajitahidi kuhimiza amani na maendeleo ya bara la Afrika 2006/01/23 Mkutano wa 6 wa wakuu wa Umoja wa Afrika unatazamiwa kufanyika tarehe 23 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Marais au viongozi wa serikali wa nchi wanachama 53 wote watahudhuria mkutano huo. Wachambuzi wanaona kuwa, kwenye mkutano huo viongozi wa nchi za Afrika watajitahidi kusukuma mbele amani na maendeleo ya bara la Afrika.
|
Iran na Syria zashirikiana kukabiliana na shinikizo la Marekani 2006/01/20 Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 19 alifika Damascus, mji mkuu wa Syria kwa ziara ya siku mbili . Hii ni mara ya kwanza kwa rais Ahmadinejad kuitembelea Syria tangu achaguliwe kuwa rais wa Syria, na huu pia ni mkutano wa pili wa wakuu wa Iran na Syria katika muda usiofikia nusu mwaka.
|
Hali ya usalama kwenye sehemu inayozalisha mafuta nchini Nigeria yazidi kuwa mbaya 2006/01/19 Kikundi cha upinzani chenye silaha, the Movement for the Emancipation of the Niger Delta, tarehe 18 kilitangaza kuwa kikundi hicho kitafanya mashambulizi kwa mashirika yote ya nchi za nje yanayochimba mafuta kwenye sehemu ya kusini nchini Nigeria.
|
Mvutano wa mataifa makubwa kuhusu suala la nyukilia la Iran 2006/01/18 Tangu Marekani kueleza mashaka yake kuhusu matumizi ya amani ya mpango wa nyukilia wa Iran, suala hilo limekuwa na utata mwingi sana, licha ya kwamba suala hilo lenyewe ni lenye utata mwingi, mvutano kati ya mataifa makubwa yanayofuatilia maslahi yake umezidisha matatizo ya suala hilo.
|
Serikali mpya ya Liberia yakabiliwa na majukumu makubwa 2006/01/17 Baada ya kumalizika vita nchini Liberia, Bibi Ellen Johnson-Sirleaf, ambaye ni rais mteule wa kwanza wa kike aliapishwa kushika wadhifa huo tarehe 16 huko Monrovia, mji mkuu wa nchi hiyo. Bibi Ellen Johnson-Sirleaf mwenye umri wa miaka 67 ni rais wa kwanza wa mwanamke aliyechaguliwa na wapiga kura katika historia ya bara la Afrika.
|
Iran yakabiliwa shinikizo kubwa duniani kuhusu suala la nyuklia 2006/01/16 Hivi karibuni Iran iliondoa lakiri zilizowekwa kwenye sehemu tatu zenye zana za nyuklia na kuanzisha upya uzalishaji wa nishati ya nyuklia. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wanataka shirika la nishati ya atomiki duniani kuitisha mkutano wa dharura kujadili suala la kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la la Umoja wa Mataifa.
|
Mpango mpya wa kiwenzi wa maendeleo ya kiuchumi usio na uchafuzi wa hewa wa Asia na Pasifiki waanzishwa 2006/01/13 Mkutano wa kuanzisha "mpango mpya wa kiwenzi wa maendeleo ya kiuchumi usio na uchafuzi wa hewa wa Asia na Pasifiki" ulimalizika tarehe 12 mjini Sydney, Australia. Mpango wenye nchi sita wa kupambna na ongezeko la joto duniani umeanzishwa.
|