Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Waziri mkuu wa China atembelea shule ya sekondari ya Congo Brazaville
  •  2006/06/21
    Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao alitembelea shule ya sekondari ya Brazaville tarehe 20 juni asubuhi kwa saa za huko. Shule hiyo inajulikana sana nchini Congo Brazavil kutokana na masomo yake ya lugha ya kichina. Ziara ya Waziri mkuu Wen Jiabao iliwafurahisha wanafunzi wa shule hiyo.
  • Hospitali ya Talangai ni uthibitisho wa urafiki kati ya China na Jamhuri ya Congo Brazaville
  •  2006/06/21
    Waziri mkuu wa serikali ya China Bw. Wen Jiabao asubuhi ya tarehe 20 mwezi Juni alikwenda kuwaangalia madaktari wa kichina wanaofanya kazi katika Hospitali ya Talangai, iliyopo Brazaville ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, ambapo alikuwa na mazungumzo na mkuu wa hospitali hiyo bibi Dimi Elisa.
  • Wen Jiabao ahudhuria sherehe ya kuzinduliwa kwa mradi wa ukarabati wa barabara nchini Ghana uliofadhiliwa na serikali ya China
  •  2006/06/20
    Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ambaye yuko ziarani nchini Ghana pamoja na rais John Kufuor wa nchi hiyo tarehe 19 juni huko Accra walihudhuria kwa pamoja sherehe ya kuzinduliwa kwa mradi wa ukarabati wa barabara nchini humo unaofadhiliwa na serikali ya China.
  • Kundi la madakatari wa China wanatoa msaada barani Afrika
  •  2006/06/20
    Bibi Chen Shuming ni dakatari wa China, hivi sasa yeye ni mmoja wa madakatari wa China wanaotoa huduma katika nchi za nje, hivi sasa anafanya kazi katika hospitali moja nchini Zimbabwe, kusini mwa Afrika. Katika kipindi hiki cha leo, nitawaletea habari kuhus kazi na maisha ya madakatari wanaotoa msaada wa huduma nchini Zimbabwe.
  • Waziri mkuu wa China afafanua kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika
  •  2006/06/19
    Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao tarehe 18 mwezi huu kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika huko Cairo, nchini Misri alifafanua masuala kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika.
  • Tutajenga nchi zetu kwa elimu tuliyopata nchini China
  •  2006/06/19
    Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao anafanya ziara rasmi ya kirafiki katika nchi za Afrika zikiwemo Misri, Tanzania, Uganda na Afrika ya Kusini tokea tarehe 17 hadi 24 mwezi Juni. Kabla ya ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao, mwandishi wetu wa habari alitembelea vyuo vikuu kadhaa vya Beijing na kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi wa nchi za Afrika, wanafunzi hao walisema, serikali ya China inazingatia sana uhusiano na Afrika na hilo ni jambo linalowahamasisha, wanatarajia kujenga nchi zao kwa kutumia elimu waliyopata nchini China.
  • Hamas yatoa ishara ya kusimamisha mapambano na Israel kwa masharti
  •  2006/06/16
    Tarehe 15 msemaji wa Hamas alisema kwamba Hamas inakubali kusimamisha mapambano na Israel kwa masharti. Wachambuzi wanaona kwamba hatua hiyo ya Hamas inasaidia kupunguza wasiwasi kati ya nchi hizo mbili, lakini pia ni vigumu kusema hali itakuwaje.
  • Urafiki kati ya China na Misri kuimarishwa siku hadi siku
  •  2006/06/16
    Mwaka huu ni mwaka wa 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Misri. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao ataanza ziara yake nchini Misri kuanzia tarehe 17 mwezi huu, na athudhuria shughuli za kuadhimisha miaka ya 50 ya uhusiano kati ya China na Misri. Misri ni kituo cha kwanza cha ziara yake katika nchi 7 za Afrika.
  • Shughuli nyingine kubwa ya kidiplomasia ya China barani Afrika
  •  2006/06/16
    Waziri mkuu wa serikali ya China Bwana Wen Jiabao atafanya ziara rasmi ya kiserekali kuanzia tarehe 17 hadi 24 mwezi huu katika nchi 7 za Afrika, nchi hizo ni Misri, Ghana, Congo Brazaville, Angola, Afrika ya kusini, Tanzania na Uganda. Lengo la ziara yake ni kuzidisha urafiki, kuongeza uaminifu, na kupanua ushirikiano ili kupata maendeleo kwa pamoja.
  • Mkutano wa 6 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Ushirikiano ya Shanghai wafanyika Shanghai
  •  2006/06/15
    Mkutano wa 6 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Ushirikiano ya Shanghai umefanyika tarehe 15 huko Shanghai, China. Wakuu wa nchi wanachama na wajumbe waliohudhuria mkutano huo wamejadili mafanikio yaliyopatikana katika maendeleo ya jumuia hiyo tangu ianzishwe miaka mitano iliyopita, wamejadili pia mwelekeo wa maendeleo ya kipindi kijacho na kutunga mpango wa ushirikiano na hatua halisi.
  • Mbona Marekani na Iraq zimeanzisha operesheni kubwa ya usalama mjini Bagdad?
  •  2006/06/15
    Kutokana na mpango wa usalama aliotoa waziri mkuu wa Iraq Bw. Nuri al-Maliki, jeshi la polisi la Iraq pamoja na jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq, tarehe 14 mwezi huu yalianzisha operesheni kubwa ya usalama, ambayo haijawahi kutokea tangu kuangushwa kwa utawala wa Sadam Hussein mwaka 2003.
  • Shirika la afya duniani lasistiza msingi wa usalama wa matumizi ya damu
  •  2006/06/14
    Tarehe 14 mwezi Juni mwaka huu ni "siku ya kutoa damu kwa kujitolea duniani". Kauli mbiu ya mwaka huu ni "ahadi": Watu wenye afya nzuri waahidi kutoa damu kwa kujitolea mara kwa mara
  • Serikali ya Bush yalaumiwa kutokana na tukio la kufa kwa wafungwa
  •  2006/06/13
    Tukio la kufa kwa wafungwa lililotokea tarehe 10 kwenye gereza la Guantanamo ni tukio la kwanza la kufa kwa wafungwa tangu lijengwe gereza hilo la jeshi la Marekani, ambalo linafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Hivi karibuni wizara ya ulinzi ya Marekani ilitangaza majina ya wafungwa hao watatu na kusema, wafungwa hao walifariki kwa kujiua. Lakini jamaa za marehemu hao walieleza mashaka yao kuhusu chanzo cha vifo vyao.
  • Shirika la kazi duniani lapiga marufuku ajira ya watoto
  •  2006/06/12
    Mkutano mkuu wa 90 wa shirika la kazi duniani uliofanyika mwezi Juni mwaka 2002, liliamua tarehe 12 Juni ya kila mwaka iwe siku ya kukomesha kutumikisha watoto duniani. Tarehe 12 Juni mwaka huu ni mwaka wa tano wa siku ya kukomesha ajira ya watoto duniani.
  • Umoja wa Ulaya wapenda kufanya mazungumzo na mashauriano ili kutatua matatizo yaliyopo kwenye ushirikiano na China katika sekta za uchumi na biashara
  •  2006/06/09
    Kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na China ni muhimu sana kwa Ulaya, Umoja wa Ulaya unapenda kufanya mazungumzo na mashauriano ili kutatua matatizo yaliyotokea katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta za uchumi na biashara.
  • "Tatizo sugu" la suala la nyuklia la Iran latazamiwa kutatuliwa
  •  2006/06/09
    Mapendekezo ya nchi sita ya kutatua suala la nyuklia la Iran yaliyowasilishwa kwa Iran hivi karibuni na mwakilishi mwandamizi anayeshughulikia mambo ya kidiplomasia na sera za nchi za nje wa Umoja wa Ulaya yanafuatiliwa sana na vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya.
  • Rais wa Kyrgyzstan afurahia mustakabali wa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai
  •  2006/06/08
    Rais Kurmanbek Bakiyev wa Kyrgyzstan hivi karibuni katika Ikulu ya Bishkek alipohojiwa na waandishi wa habari wa vyombo 6 vya habari vya China kikiwemo cha Radio China Kimataifa, alijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu mkutano utakaofanyika huko Shanghai wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, pamoja na ziara ya kiserikali atakayofanya hivi karibuni nchini China.
  • Suala la nyukilia la Iran lakabiliwa na fursa mpya ya utatuzi wa kidiplomasia
  •  2006/06/07
    Katibu wa kamati ya usalama ya Iran, ambaye ni mwakilishi wa kwanza katika mazungumzo ya suala la nyukilia, Bw. Ali Lirijani tarehe 6 huko Teheran, mji mkuu wa Iran alisema, mpango mpya wa mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 6 kuhusu utatuzi wa suala la nyukilia la Iran ni wenye hatua mwafaka.
  • Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai hakika utapata mafanikio mema
  •  2006/06/07
    Mkutano wa 6 wa Baraza la wakuu wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai unatazamiwa kufanyika huko Shanghai, China kuanzia tarehe 15 mwezi huu.
  • Mazungumzo ya kitaifa ya Palestina yashindwa, Bwana Abbas atafuta upigaji kura za maoni ya raia
  •  2006/06/06
    Ofisa wa Chama cha ukombozi wa taifa cha Palestina Bwana Azzam al Ahmad tarehe 5 usiku wa manane alitangaza huko Ramallah kuwa, kwenye mkutano wa mazungumzo ya kitaifa ya Palestina uliofanyika usiku huo, pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano hazikuweza kufikia "makubaliano ya gerezani".
  • Mgongano kati ya Fatah na Hamas kufikia kikomo
  •  2006/06/05
    Ofisa wa kundi la chama cha ukombozi wa taifa cha Palestina (Fatah), tarehe 4 alisema endapo kundi la Hamas hakitakubali mapendekezo ya kisiasa ya kuanzisha nchi kwenye ardhi ya Palestina inayokaliwa, mwenyekiti wa mamlaka ya taifa ya Palestina Bw. Mahmoud Abbas ataamua ufanyike upigaji kura kuhusu mapendekezo hayo.
  • Nchi tano wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama na Ujerumani zafikia makubaliano kuhusu suala la nyuklia la Iran
  •  2006/06/02
    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tano wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama na Ujerumani tarehe mosi Juni walikutana huko Vienna na kufikia makubaliano kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya kuhusu utatuzi wa suala la nyuklia la Iran.
  • Kwanini Marekani imekubali kuwa na mazungumzo na Iran
  •  2006/06/01
    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleezza Rice tarehe 31 mwezi Mei alitangaza kuwa, kama Iran itaacha kusafisha uranium na urudishaji nishati ya nyukilia, Marekani itafikiria kushirikiana nayo na kuwa na mazungumzo kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya
  • Udhibiti wa uvutaji sigara ni jukumu kubwa na gumu
  •  2006/05/31
    Tarehe 31 mwezi Mei mwaka huu ni siku ya kutovuta sigara duniani ya mwaka wa 19. Kauli mbiu ya siku hiyo ya mwaka huu ni "tumbaku inaua".
  • Mpango mpya kuhusu suala la nyukilia la Iran kujadiliwa Vienna
  •  2006/05/30
    Wawakilishi wa nchi 5 wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na mwakilishi wa Ujerumani watakuwa na mkutano tarehe 1 mwezi Juni kuhusu mpango mpya wa utatuzi wa suala la nyukilia la Iran uliotolewa na Umoja wa Ulaya.
  • China kuchukua hatua kuinua ufanisi wa matumizi ya raslimali ya maji
  •  2006/05/29
    Mkutano wa taifa wa kazi kuhusu rasilimali ya maji, ambao unafanyika hivi sasa kwenye mji wa Eerduosi, mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulioko sehemu ya kaskazini mwa China, tarehe 28 ulitoa wito wa kutaka kuchukuliwa hatua zaidi katika miaka mitano ijayo
  • Jumuiya ya kimataifa yafanya juhudi kusaidia sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi nchini Indonesia
  •  2006/05/29
    Baada ya tetemeko la ardhi kutokea katika Mkoa wa Java ya Kati wa Indonesia na kusababisha vifo na majeruhi ya watu elfu kadhaa, jumuiya ya kimataifa imeanzisha kwa haraka harakati za uokoaji na utoaji misaada
  • Zimbabwe yafanya kongamano la kuadhimisha Siku ya Afrika
  •  2006/05/26
    Ili kuadhimisha tukio la kuanzishwa  kwa jumuiya ya nchi huru za Afrika,  mabalozi wa nchi za Afrika nchini Zimbabwe na Chuo Kikuu cha Harare walifanya kongamano kwa pamoja ili kuadhimisha siku hiyo.
  • Mkutano kuhusu suala la nyukilia la Iran wafanyika mjini London
  •  2006/05/25
    Maofisa wa ngazi ya juu wa nchi 6 zikiwemo nchi 5 za wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambazo ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia na China, pamoja na Ujerumani, walikuwa na mkutano wa faragha tarehe 24 huko London, wakijadili mpango mpya uliopendekezwa na nchi 3 za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wenye lengo la kuihimiza Iran iache mpango wake wa nyukilia.
  • Ziara ya chansela wa Ujerumani itasukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani
  •  2006/05/24
    Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel alifanya ziara nchini China kuanzia tarehe 21 hadi 23 mwezi huu, ziara yake hiyo ilivutia macho ya watu wengi, kwani hii ni ziara ya kwanza ya chansela huyo nchini China tangu ashike madaraka mwezi  Novemba mwaka jana.
    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44