Bei ya nafaka inayopanda kwa kasi duniani inaleta hali mbaya 2008/04/10 Mkuu wa Benki ya Dunia Bw. Robert Zoellick hivi karibuni ameonya kwamba bei ya nafaka inayopanda kwa kasi imesababisha baadhi ya nchi kukabiliwa na tishio la njaa, na kuzifanya baadhi ya nchi zinazoendelea zipoteze mafanikio yao yaliyoptikana katika juhudi za miaka kadhaa katika mapambano yao dhidi ya umaskini. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon pia amekuwa na wasiwasi kuhusu kupanda huko kwa bei.
|
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan kutembelea China 2008/04/09 Kutokana na mwaliko wa rais wa China Hu Jintao, rais Pervez Musharraf wa Pakistan atafanya ziara ya siku 6 nchini China kuanzia tarehe 10. Tarehe 8 alizungumza na waandishi wa China kuhusu ziara yake.
|
Kwa nini majeshi ya Marekani na Iraq yamelishambulia "jeshi la Mehdi" 2008/04/08 Hivi karibuni jeshi la Marekani na jeshi la usalama la Iraq yalifanya mashambulizi mfululizo dhidi ya jeshi la wanamgambo la "Mehdi" la madhehebu ya Shia katika sehemu ya Basra, sehemu ya kusini ya Iraq. Mashambulizi hayo yaliyoanza tarehe 25 Machi sasa yameingia katika wiki ya tatu.
|
Putin na Bush wafanya mazungumzo ya kuagana 2008/04/07
Rais Vladimir Putin wa Russia na rais George W. Bush wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Russia, tarehe 6 walifanya mazungumzo huko Sochi, mji wa kusini mwa Russia. Kutokana na kuwa rais Putin atamaliza muda wake wa urais mwezi Mei mwaka huu, vyombo vya habari vinayaita mazungumzo hayo kama ni mazungumzo ya kuagana kati ya wakuu hao wawili. Baada ya mazungumzo hayo, nchi hizo mbili zilitoa taarifa kuhusu uhusiano wa kimkakati kati ya Russia na Marekani.
|
Chama cha upinzani cha Zimbabwe chashinda kwenye uchaguzi wa baraza la chini la bunge la nchi hiyo 2008/04/04 Jioni ya tarehe 3 mwezi Aprili tume ya uchaguzi ya Zimbabwe ilianza kutangaza matokeo ya uchaguzi wa baraza la juu la bunge la nchi hiyo. Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa baraza la chini la bunge, Chama cha harakati za mabadiliko ya kidemokrasia (MDC) ambacho ni chama kikubwa cha upinzani nchini humo kilikishinda Chama cha ZANU-PF kinachoongozwa na rais wa sasa Robert Mugabe. Na matokeo ya uchaguzi wa rais bado hayajatangazwa.
|
Jumuiya zisizo za kiserikali zafanya juhudi kushiriki kwenye kampeni ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa 2008/04/03 Mazungumzo ya siku 5 kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kufanyika huko Bangkok, Thailand, wajumbe 1200 kutoka nchi 163 wanahudhuria Mkutano huo. Mkutano huo unajadili hasa namna ya kutekeleza "mpango wa Bali" uliopitishwa mwaka jana kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.
|
Majadiliano kuhusu mada maalumu kuhusu kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia yafanyika 2008/04/02 Majadiliano ya siku mbili ya mada maalum kuhusu kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia yanafanyika kuanzia tarehe 1 Aprili kwenye Baraza kuu la 62 la Umoja wa Mataifa, ambapo wajumbe wanajadili hasa namna ya kuhimiza malengo ya maendeleo ya milenia yatimizwe mapema iwezekanavyo
|
China yahimiza ushirikiano wa eneo dogo la mto mkubwa Mekong 2008/04/01 Kutokana na mwaliko wa waziri mkuu wa Laos Bw. Bouasone Bouphavanh, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alifanya ziara nchini Laos na kuhudhuria mkutano wa 3 wa viongozi wa ushirikiano wa eneo dogo la mto mkubwa Mekong(GMS) uliofanyika mjini Vientiane kuanzia tarehe 29 hadi tarehe 31 mwezi Machi.
|
Mazungumzo ya duru jipya kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yaanza tena mjini Bangkok 2008/04/01 Mazungumzo ya duru jipya ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yalianza tena tarehe 31 mjini Bangkok. Hayo ni mazungumzo ya kwanza kufanyika baada ya "Ramani ya Bali" iliyopitishwa mwezi Desemba kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.
|
Bw. Li Changchun atembelea kituo cha utamaduni na michezo cha vijana cha El Menzah cha Tunisia 2008/03/31 Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Li Changchun ambaye yuko ziarani nchini Tunisia tarehe 30 Machi alitembelea Kituo cha utamaduni na michezo cha vijana cha El Menzah ambacho kilijengwa kwa msaada wa China
|
Maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe yakamilika 2008/03/28 Tarehe 29 Zimbabwe itafanya uchaguzi mkuu, uchaguzi wa bunge na uchaguzi wa serikali za mitaa. Hivi sasa maandalizi yote yamekamilishwa na uchaguzi huo umeanza kupiga hodi. Serikali ya Zimbabwe inataka uchaguzi huo uwe wa haki, uadilifu na utulivu, zaidi ya wito huo serikali imetoa sheria maalumu ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani.
|
Uchaguzi mkuu wa Zimbabwe utakuwa na mabadiliko mengi 2008/03/27 Tarehe 29 Zimbabwe itafanya uchaguzi mkuu, uchaguzi wa bunge na uchaguzi wa serikali za mitaa. Uchaguzi huo unafanyika katika hali ambayo uchumi wa nchi hiyo umedumaa kwa miaka saba mfululizo, na kuwekewa vikwazo na nchi za magharibi kwa miaka mingi, kwa hiyo matokeo ya uchaguzi huo yatakuwa na athari kubwa kwa mustakbali wa Zimbabwe.
|
Jeshi la Iraq lafanya operesheni kabambe dhidi ya "Jeshi la Mehdi" 2008/03/26 Alfajiri ya tarehe 25 jeshi la Iraq lilianza operesheni kabambe katika mji mkubwa wa pili wa Iraq Basra, lakini lengo la operesheni hiyo sio magaidi bali ni kundi la wanamgambo "Jeshi la Mehdi". Habari zinasema operesheni hiyo ni kubwa kabisa katika miaka yote mitano tokea vita vya Iraq kuzuka.
|
Bw. Li Changchun afanya mazungumzo na wanafunzi wa Algeria waliorudi kutoka China 2008/03/25 Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Li Changchun ambaye yuko ziarani nchini Algeria, tarehe 24 kwenye hoteli aliyofikia alifanya mazungumzo na wanafunzi wa nchi hiyo waliorudi kutoka China.
|
Kujenga daraja la urafiki kati ya China na Algeria 2008/03/24 Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bwana Li Changchun tarehe 23 mchana alikagua kiwanja cha ujenzi wa barabara ya kasi inayoanzia mashariki hadi magharibi nchini Algeria ambayo inajengwa na kampuni ya China.
|
Serikali ya Uingereza ina matatizo ya kufanya uamuzi wa kuondoa jeshi lake kutoka nchi ya Iraq 2008/03/21 Tarehe 20 Machi ni siku ya kutimiza miaka mitano tokea Uingereza iifuate Marekani kutuma jeshi kuingia nchini Iraq. Siku hiyo waziri mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown alikutana na mbunge wa Baraza la Juu la Marekani Bw. John McCain na pande mbili zilijadiliana kuhusu suala la Iraq.
|
Vilio vya raia wa Iraq 2008/03/20 Tarehe 20 Machi miaka mitano iliyopita, pamoja na mlio wa king'ora jeshi la Marekani lilianzisha vita dhidi ya Iraq. Leo baada ya miaka mitano kupita vita hivyo vinavyoongozwa na Marekani licha ya kutatua suala la Iraq, vimeizamisha nchi hiyo kwenye hali mbaya zaidi
|
Jumuiya ya kimataifa yaendelea kuhimiza utatuzi wa suala la Darfur 2008/03/19 Mkutano wa majadiliano yasiyo ya rasmi kuhusu utatuzi wa suala la Darfur ambao ulianzishwa kwa pamoja na mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Darfur Bw. Jan Eliasson na mjumbe maalum wa suala hilo wa Umoja wa Afrika Bw. Salim Ahmed Salim, ulimalizika tarehe 18 Machi huko Geneva, Uswisi
|
Kwa nini Bw. Cheney alifanya ziara ya ghafla nchini Iraq? 2008/03/18 Wakati tarehe 20 Machi mwaka huu ambayo ni mwaka ya 5 ya kuanzishwa kwa vita vya Iraq inapokaribia, makamu wa rais wa Marekani Bw. Dick Cheney tarehe 17 mwezi huu alifanya ziara ya ghafla nchini Iraq bila kutangaza habari yoyote. Bw. Cheney akiwa ni mpangaji wa vita hivyo, maoni aliyotoa katika ziara hiyo kuhusu vita vya Iraq yanafuatiliwa sana.
|
Mkutano wa mawaziri kuhusu masuala ya mazingira wafungwa 2008/03/17 Mkutano wa nne wa mawaziri wa kundi la nchi 20 kuhusu masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, nishati isiyo na uchafuzi na maendeleo endelevu, ulifanyika kwa siku 2 na kufungwa tarehe 16 katika Chiba, Japan. Mkutano huo ni sawa na mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa wa mwaka uliopita
|
Mwelekeo wa uchaguzi wa bunge la Iran 2008/03/14 Uchaguzi wa 8 wa bunge la Iran utafanyika rasmi tarehe 14, lakini inaonekana kuwa watu hawafuatilii sana uchaguzi huo. Wachambuzi wanasema, kwa kuwa watu wengi wa kundi la mageuzi wamefutiwa haki ya kushiriki kwenye uchaguzi huo, hivyo kundi la wahafidhina bado watapata viti vingi zaidi, na kuendelea kudhibiti bunge. Bunge la Iran ni chombo cha ngazi ya juu kabisa cha utungaji wa sheria.
|
Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya wafuatilia mambo ya uchumi 2008/03/13 Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya wa majira ya spring, ambao utafanyika kwa siku mbili, umepangwa kuanza usiku wa tarehe 13 kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels. Mkutano huo utafuatilia zaidi mambo ya uchumi yakiwemo masuala mawili ya mpango wa utekelezaji wa "mkakati wa Lisbon" katika miaka mitatu ijayo, pamoja na hatua za kukabiliana na mgogoro kwenye soko la fedha.
|
Marekani na Iraq zaanza kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili 2008/03/12 Wizara ya mambo ya nje ya Iraq tarehe 11 ilitangaza kuwa wajumbe wa nchi hiyo na Marekani wameanza kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa kudumu kati ya nchi hizo mbili. Kwenye mazungumzo tatizo sugu ni suala la jeshi la Marekani nchini Iraq.
|
Nguvu za China kwenye maonesho ya magari ya Geneva 2008/03/10 Wapendwa wasikilizaji, maonesho ya kimataifa ya 78 ya magari ya Geneva yalifunguliwa tarehe 6 mwezi Machi. Katika maonesho ya safari hii ya siku 11, wafanyabiashara zaidi ya 260 kutoka nchi zaidi ya 30 wameshiriki maonesho hayo, na kuonesha teknolojia zao za kisasa pamoja na aina mpya za magari yao, kati ya magari yanayooneshwa kwenye maonesho ya Geneva kuna magari ya BYD na Brilliant ya China.
|
Tukio kubwa la shambulizi la kigaidi latokea Jerusalem 2008/03/07 Tukio la shambulizi la kigaidi lilitokea tarehe 6 usiku kwenye shule moja ya dini ya kiyahudi huko Jerusalem, na kusababisha vifo vya wanafunzi wanane na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa. Tukio hilo ni la shambulizi la kigaidi lililosababisha vifo na majeruhi ya watu wengi zaidi huko Jerusalem tokea mwaka 2004.
|
OPEC yaamua kudumisha kiwango cha utoaji mafuta 2008/03/06 Msemaji wa jumuiya ya nchi zinazotoa mafuta ya petroli duniani(OPEC), ambayo hivi sasa inafanya mkutano huko Vienna, Bw. Ibrahim Hussein, tarehe 5 alitangaza kuwa mkutano wa 148 wa mawaziri wa nchi za OPEC umeamua kudumisha kiwango cha utoaji mafuta cha hivi sasa. Hii ni mara ya pili kwa OPEC kuamua kudumisha kiwango cha utoaji wa mafuta ya petroli ili kukabiliana na shinikizo kutoka baadhi ya nchi ikiwemo Marekani baada ya mkutano wa mawaziri wa mwezi Februari.
|
China yashiriki kwenye maonesho ya teknolojia ya mawasiliano ya habari duniani 2008/03/05 Maonesho makubwa ya sayansi na teknolojia ya duniani, ambayo ni maonesho ya teknolojia ya upashanaji habari ya Hannnover ya Ujerumani (CeBIT), yalifunguliwa tarehe 4 mwezi Machi, maonesho hayo yenye eneo la mita za mraba laki 2.4, yalishirikisha kampuni na viwanda 584 kutoka nchi na sehemu 77 za duniani. Ofisa mmoja husika wa China alisema, bidhaa nyingi zaidi zinazooneshwa na China kwenye maonesho hayo ni za elektroniki
|
Wafanyakazi wa Darfur kwenye Shamba la Khartoum 2008/03/04 Kwenye kitongoji cha Khartoum, mji mkuu wa Sudan, kuna shamba moja linaloendeshwa na Wachina, wafanyakazi wa shamba hilo wote wanatoka kutoka sehemu ya Darfur. Kwa kufanya kazi huko wanaweza kukidhi mahitaji ya familia zao na huku wanatoa mchango kuendeleza shamba hilo
|
Jeshi la kulinda amani la China lililoko Darfur 2008/03/03 Mwezi Novemba, mwaka 2007, maofisa na askari wa uhandisi wa kikosi cha kwanza cha China cha kulinda amani huko Darfur, waliwaaga watu wa familia zao na kuondoka China, kwenda kutekeleza jukumu la kulinda amani huko Darfur walilokabidhiwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
|
Serikali ya Kenya na chama cha upinzani vyasaini makubaliano kuhusu kuunda serikali ya muungano 2008/02/29 Chini ya uendeshaji wa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan, serikali ya Kenya na chama cha upinzani vilifanya mazungumzo ya wiki kadhaa, tarehe 28 viliafikiana na kusaini makubaliano kuhusu kuunda serikali ya muungano.
|